Usafi wa mtayarishaji wa chakula
Osha mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka na ya kutosha,
kabla ya kutayarisha chakula au baada ya kutoka chooni.
Hakikisha usafi wa mwili na nguo.
Funga vidonda vilivyoko kwenye mikono wakati wa
kutayarisha chakula
.
Usafi wa vyombo
Osha sawasawa vyombo vilivyotumika kutayarishia
vyakula vibichi hasa nyama, samaki, au mayai kabla
ya kuvitumia kutayarishia vyakula vingine.
Ni muhimu kuwa na kichanja cha kuanikia vyombo.
Hakikisha sehemu ya kuhifadhi vyombo ni safi na
kavu.
Usafi wa sehemu ya kutayarishia
chakula
Hakikisha jiko au sehemu ya kutayarishia
chakula ni safi.
Kusanya uchafu na mabaki ya vyakula na
kuyatupa kwenye shimo la taka au kwenye
chombo kilichofunikwa.
Usafi na usalama wa chakula
Hakikisha vyakula hasa vile vya aina ya nyama,
samaki au mayai vimepikwa na kuiva sawasawa.
Chakula kiliwe kingali cha moto.
Osha matunda na mboga-mboga kwa maji safi na
ya kutosha.
Epuka kutumia nafaka au vyakula vilivyooza,
vilivyoota ukungu, au vilivyoharibika
Epuka kula viporo. Inapobidi kutumia kiporo, ni
muhimu kupasha moto mpaka kichemke.
v Hakikisha hakuna mwingiliano wa vyakula vilivyopikwa na vibichi ili kuepuka kuingiliwa na
vimelea vya maradhi (sibiko).
Epuka kutumia vyakula vilivyopita muda wa matumizi (expiry date).
Epuka kununua mayai yenye ufa, mboga-mboga au matunda yaliyoanza kuharibika.
Usafi na usalama wa maji ya kunywa
Chemsha maji ya kunywa na yahifadhi katika
chombo safi kilichofunikwa.
Hakikisha chombo kinachotumika kuchotea maji
ya kunywa ni safi na kisitumike kunywea maji.
Tumia maji yaliyochemshwa kutengenezea juisi
au barafu.
No comments:
Post a Comment