kevin

kevin
120*120

Thursday, December 15, 2011

USAFI NA USALAMA WA CHAKULA NA MAJI

Usafi wa mtayarishaji wa chakula

Osha mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka na ya kutosha,
kabla ya kutayarisha chakula au baada ya kutoka chooni.
 Hakikisha usafi wa mwili na nguo.
 Funga vidonda vilivyoko kwenye mikono wakati wa
kutayarisha chakula
.
Usafi wa vyombo

Osha sawasawa vyombo vilivyotumika kutayarishia
vyakula vibichi hasa nyama, samaki, au mayai kabla
ya kuvitumia kutayarishia vyakula vingine.
 Ni muhimu kuwa na kichanja cha kuanikia vyombo.
 Hakikisha sehemu ya kuhifadhi vyombo ni safi na
kavu.

Usafi wa sehemu ya kutayarishia
chakula


Hakikisha jiko au sehemu ya kutayarishia
chakula ni safi.
 Kusanya uchafu na mabaki ya vyakula na
kuyatupa kwenye shimo la taka au kwenye
chombo kilichofunikwa.

Usafi na usalama wa chakula


 Hakikisha vyakula hasa vile vya aina ya nyama,
samaki au mayai vimepikwa na kuiva sawasawa.
 Chakula kiliwe kingali cha moto.
 Osha matunda na mboga-mboga kwa maji safi na
ya kutosha.
Epuka kutumia nafaka au vyakula vilivyooza,
vilivyoota ukungu, au vilivyoharibika
 Epuka kula viporo. Inapobidi kutumia kiporo, ni
muhimu kupasha moto mpaka kichemke.
v Hakikisha hakuna mwingiliano wa vyakula vilivyopikwa na vibichi ili kuepuka kuingiliwa na
vimelea vya maradhi (sibiko).
 Epuka kutumia vyakula vilivyopita muda wa matumizi (expiry date).
 Epuka kununua mayai yenye ufa, mboga-mboga au matunda yaliyoanza kuharibika.

Usafi na usalama wa maji ya kunywa


 Chemsha maji ya kunywa na yahifadhi katika
chombo safi kilichofunikwa.
 Hakikisha chombo kinachotumika kuchotea maji
ya kunywa ni safi na kisitumike kunywea maji.
 Tumia maji yaliyochemshwa kutengenezea juisi
au barafu.

Friday, December 2, 2011

VYAKULA NA PRESHA


  VIJUE VYAKULA VYA MGONJWA WA PRESHA 


Hakuna kitu kibaya kwa mgonjwa kama kula vyakula ambavyo huongeza tatizo alilonaalo bila kujijua. Kwa kuwa tunaamini kwamba, jinsi tulivyo tunatokana na tunavyokula, basi kupona au kuendelea kuugua nako kutategemea sana vyakula tutakavyokula.

Vyakula viko vya aina mbalimbali na kila kimoja kina umuhimu wake katika mwili wa binadamu. Lakini mtu ukishakuwa mgonjwa, hasa wa maradhi sugu kama vile presha, kisukari, ukimwi, n.k, ni lazima ujue vyakula gani unapaswa kula na vyakula gani unapaswa kuviepuka.

Leo tunaangalia vyakula anavyopaswa kuvila ama kuviepuka mgonjwa wa shinikizo la juu la damu (High Blood Pressure). Kama inavyojulikana, maradhi haya hutokana na staili ya maisha anayoishi mtu, vivyo hivyo hata udhibiti wake utategemea na atakavyoishi.

NYAMA NA MAYAI
Nyama na mayai ni adui mkubwa wa mgonjwa wa presha. Ni wagonjwa wangapi wanafahamu kwamba vyakula hivi ni hatari kwa maisha yao na wakaacha kabisa kuvitumia? Naamini ni wachache sana wanaolifahamu hili na kulizingatia, hasa ukizingatia utamu wa vyakula hivyo.

Inaelezwa kuwa katika vyakula ambavyo mgonjwa wa presha akivila huchangia kupandisha presha ni mayai na nyama, hasa ile itokanayo na ng’ombe, mbuzi, nguruwe na nyingine za jamii hiyo.

ZINGATIA VYAKULA HIVI
Ukisha kuwa mgonjwa wa presha, ulaji wa vyakula vitokanavyo na nafaka halisi, matunda na mboga za majani, linakuwa suala la lazima na siyo hiyari. Mgonjwa wa presha anashauriwa kula zaidi vyakula hivyo na kupunguza ulaji wa vyakula vyenye protini nyingi, ikiwemo nyama kama ilivyoolezwa awali.

Katika orodha ndefu ya matunda anayopaswa mgonjwa kula na kupata nafuu, ni pamoja na hii ifutayao, ambayo huweza kutumika pia kama tiba, kwani matunda haya yameonekana kuwa na virutubisho vingi zaidi vinavyoweza kudhibiti presha:

Vitunguu saumu
Kula vitunguu saumu kwa wingi, hutoa nafuu kubwa kwa mgonjwa. Unaweza kula punje mbili hadi tatu kwa siku na kuchanganya kwenye mboga pia.
Limau
Pia penda kula limau mara kwa mara, nalo ni miongoni mwa matunda yanayotoa nafuu kwa mgonjwa wa presha. Limau lina Vitamin P ambayo utaipata kwa kunywa juisi yake au nyama na maganda yake.

Zabibu mbivu
Zabibu nazo zimeorodheshwa miongoni mwa matunda anayotakiwa kula mgonjwa wa presha ili kupata nafuu, nayo yana vitamin P ambayo huzuia kuziba kwa mishipa ya damu.

Tikiti maji
Tikitimaji nalo ni miongoni mwa matunda anayopaswa kula mgonjwa wa presha. Halikadhalika, mbegu za tikiti maji zinaweza kutengenezwa na kuliwa kama dawa inayoweza kumpa nafuu kubwa mgonjwa. Kausha mbegu zake, kisha zikaange, ziliwe mara kwa mara kama karanga.

Mchele
Mchele una kiwango kidogo cha ‘fat’ na pia una kiwango kidogo cha ‘kolestrol’, hivyo kukifanya kuwa chakula bora kwa mgonjwa wa presha. Hivyo wali ni sawa kuliwa na mgonjwa wa presha, hasa ukipata ule mchele usioondolewa virutubisho vyake (brown rice).

Viazi vitamu
Viazi vitamu, hasa vile vya kupika na maganda yake, vinafaa sana kuliwa na mgonjwa wa presha kwani vina madini mengi ya ‘potasiamu’ na havina madini chumvi.

Juisi ya mboga majani
Ulaji wa mchanganyiko wa juisi ya mboga, hasa karoti na mchicha (spinach) ni mzuri sana kwa mgonjwa wa presha, huweza kutumika pia kama tiba. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili au tatu.

Kwa kuzingatia ulaji wa vyakula vilivyoainishwa hapo juu na kufanya mazoezi mara kwa mara, mgonjwa wa presha anaweza asisumbuliwe kabisa na tatizo hilo na kujihisi kupona hata bila kutumia dawa. Hata hivyo, hilo linawezekana tu iwapo utajitambua mapema na kuanza kuchukua hatua za ulaji sahihi wa vyakula sasa na siyo baadaye!