Ndugu wapendwa ni mataumaini yangu kuwa mu wazima, poleni sana na mihangaiko ya hapa na pale ya kimaisha.
Leo ningependa kuleta kijiweni mada ihusuyo vyakula tulavyo na virutubisho tuvipatavyo:
Chakula hutupa nguvu na virutubishi ambavyo mwili huhitaji ili kudumisha afya na maisha,kukua na kustawi, kusonga, kuchapa kazi kucheza na kujifunza.
Mwili huhitaji virutubishi vya aina nyingi - protini, wanga, mafuta, na madini - na hivi hutokana na vyakula tulavyo.
- Protini zinahitajika kujenga na kudumisha misuli, damu, ngozi na tishu na viungo mwilini.
- Wanga na mafuta kimsingi hutupa nguvu, ingawa mafuta mengine pia huhitjika kama vifaa vya ujenzi na kuusaidia mwili kutumia baadhi ya vitamini.
- Vitamini na madini huhitajika kwa viwango vidogo zaidi kuliko protini, mafuta na wanga, lakini navyo ni muhimu kwa lishe bora. Vinasaidia mwili kufanya kazi vizuri na kuwa wenye afya. Baadhi ya madini pia huwa sehemu ya tishu za mwili, kwa mfano, kalisiamu na floridi ilyo katika mifupa na meno na chuma hupatikana katika damu.
- Utembo na maji safi pia huhitaji kwa maakuli mazuri.
Vyakula vyote vina virutubishi lakini vyakula mbalimbali huwa pia na tofauti vya virutubishi mbalimbali.
- Vyakula vyenye wingi wa protini ni aina zote za nyama, kuku, samaki, maharagwe, dengu, maharagwe soya, njugu, maziwa, chizi, maziwa mgando na mayai.
- Vyakula vyenye wingi wa kabohidrati ni mchele, mahindi, ngano na nafaka, aina zote za viazi vikuu na mzizi yenye kabohidrati na sukari.
- Vyakula vyenye wingi wa Shahamu ni mafuta, baadhi ya nyama na bidhaa za nyama, mafufa ya nguruwe, siagi, samli na baadhi ya bidhaa za maziwa, siagi kutokana na ute wa njugu, baadhi ya aina za samaki, vyakula vya jamii ya njugu nasoya.
- Vyakula vyenye wingi wa vitamini A ni mboga zenye kijani kilichokolea, karati, viazi vitamu vyenye njano iliyokolea, boga, embe, papai, mayai na ini.
- Vyakula venye kijani kilichokolea , jungu, maharagwe, mbaazi, nafaka, nyama, samaki na mayai.
- Vyakula vyenye wingi wa vitamini C ni matunda na kiasi kikubwa cha mboga, pamoja na viazi.
- Vyakula vyenye wingi wa ayani ni nyama, samaki, njugu, maharagwe, mbaazi, mboga zenye matawi ya kijani kilichokolea na matunda yaliyokaushwa.